
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mpinga alisema kuwa baada ya
mtuhumiwa kufanya kitendo hicho alikimbia kusikojulikana na wasamaria
wema waliwakuta waathirika wakiwa katika hali mbaya na kuwapeleka katika
Hospitali ya Rufani ya Mbeya kwa ajili ya kupata matibabu.
Kamanda Mpinga alieleza kuwa juhudi za kumtafuta mtuhumiwa kwa
kushirikiana na mume wa muathirika huyo aliyefahamika kwa jina la Lausi
Kidagile ambaye naye ni mkazi wa Sae zinaendelea.
“Jeshi la Polisi linalaani vikali kitendo hicho na tunaomba mwananchi
yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kumkamata mtuhumiwa atupatie
ili hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Kamanda Mpinga.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamsaka
mtuhumiwa huyo, Emmy Kyando (40, mkazi wa Sai jijini Mbeya ambaye
aliwafanyia kitendo hicho cha kinyama watu hao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga, aliwataja wengine
waliomwagiwa tindikali kuwa ni Loveness John (11), mwanafunzi wa darasa
la sita katika Shule ya Msingi Sinde na Nancy Peter (5), wakazi wa Mtaa
wa Mwanshinga, Kata ya Manga jijini Mbeya.
Walimwagiwa na kujeruhiwa na tindikali hiyo usoni, kifuani na mikononi Julai 19, mwaka huu saa tatu usiku.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufani Kanda ya Mbeya, Goodlove Mbwanji,
alithibitisha kuwapokea wagonjwa katika hali mbaya hususani mama wa
watoto Shangema, akiwa ameharibika usoni na macho kutokuona kabisa huku
mtoto Loveness akiendelea kupata matibabu na afya yake kuimarika pamoja
na Nancy ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.
Mbwanji alisema wanaendelea na matibabu kwa mama huyo na kwamba idara
ya upasuaji pamoja na madaktari wengine bingwa wamemuwekea uangalizi
mzuri ili apate matibabu stahiki.
chanzo: zanzibar24.
Comments