Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa tahadhari kuwa, dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa zinaa wa kisonono, zimeanza kupata usugu na huenda zisiweze kutibu tena ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika mataifa 77 tofauti Duniani, WHO imebaini kuwa dawa za kisonono zimeshindwa kutibu ugonjwa huo katika nchi za Japan, Ufaransa na Uhispania.
Hata hivyo, shirika hilo linasema wengi wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi masikini ambazo zina vifaa duni vya kudhibiti ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa WHO wanaofanya mapenzi bila kinga wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
chanzo:Mwananchi.
Comments