Waziri wa kilimo, mifugo atoa agizo kwa watendaji wa wizara yake kufanya utafiti juu ya maeneo yanayofaa kwa kilimo cha korosho Pemba.

Related imageWaziri wa kilimo, mifugo, mali asili na uvuvi Zanzibar Mh, Hamad Rashid  Moh'd amewagiza  maafisa wa wizara  hiyo  kushirikiana na idara ya misitu kuyapima na kuyafanyia utafiti maeneo  ya micheweni, giningi na kifundi ili kulima zao la korosho.

Amesema  sehemu hizo zina maeneo mazuri yanayoonesha kustawi vizuri  zao la korosho  ambalo na  muhimu duniani.

Agizo hilo ameliutoa  mapema leo huko Giningi  Chambani  Mkoa wa Kusini Pemba alipokua katika ziara yake ya siku mbili kisiwani humo na kubahatika kutembelea eneo hilo ambalo lilikuwa likitumika kwa uchimbaji wa mchanga.


Waziri Hamadi amesema iwapo  wizara itafanya kazi hiyo kwa ufani  mkubwa  ya kuipanda mikorosho ya kisasa basi muda mfupi itaiwezesha serikali kujipotia mapato kupitia zao hilo mbayo yatasaidia kuendesha shughuli nyengine za  kiuchumi.

Sambamba na hayo waziri huyo ameitaka wizara hiyo kutokuwafumbia macho wale wote ambao wanahujumu mali asili ambazo ni muhimu katika kujenga uchumi wa nchi yetu hata kama wapo ndani ya wizara hiyo.

Amesema kuwa serikali  haipo tayari kuona kuwa kuna badhi ya watu wanazihujumu mali asili na bado wanaendelea kubembelezwa.

Waziri Hamad ambaye yopo Pemba kwa ziara ya kuangalia utendaji wa wizara yake pia amebahatika kutembelea katika kiwanda cha kukamua wa  mafuta ya halizeti kilichopo Dodeani .

Comments