WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kutoruhusu
wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa
elimu umetolewa kwa mujibu wa Sheria na sio utaratibu mpya kama
inavyopotoshwa na baadhi ya wanaharakati.
Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo jana (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge mjini Dodoma.
Alisema
msimamo huo wa kisheria unalenga kuwafanya watoto wa kike
wajishughulishe na masomo yao zaidi badala ya kushiriki kwenye vitendo
vya ukiukwaji wa maadili.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015, jumla ya wanafunzi 3,637 waliacha masomo kutokana na kupata ujauzito.
“Kuwaachisha
masomo wanafunzi waliopata ujauzito ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni
za Elimu za mwaka 2002, zinazoruhusu kufukuza na kuondoa wanafunzi
shuleni kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo uasherati, wizi, ulevi,
kutumia dawa za kulevya pamoja na utoro.”
“Lengo
hili lina nia ya kuwahimiza wazazi wawafundishe watoto wao mambo mema
ndani ya familia na wawakataze kushiriki vitendo vya ngono katika umri
dhamira ya Serikali ni kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu kwa ajili
ya manufaa yake na Taifa kwa ujumla.”
Waziri
Mkuu alisema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wote
wanapata elimu. Hivyo ni lazima tuhakikishe mtoto wa kike anapata elimu
stahiki na masomo yake hayakatizwi kwa kupata ujauzito.”
Alisema
Serikali imewekeza kwenye mtoto wa kike, ambapo kifungu Na. 60 (b) cha
Sheria ya Elimu Sura ya 353, kinatoa adhabu ya miaka 30 jela kwa yeyote
atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi.
Pia,
sheria inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela au faini ya
shilingi milioni tano, au vyote kwa pamoja kwa anayeshiriki kumuozesha
mtoto wa shule.
“Natoa
wito kwa Wakuu wa Wilaya kusimamia utekelezaji wa Sheria za nchi zenye
lengo la kumlinda mtoto wa kike. Aidha, nawashauri Waheshimiwa Wabunge,
mshirikiane na Halmashauri zenu kuweka mikakati ya kudhibiti ujauzito
kwa watoto wa shule.”
Wahamasisheni
wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola, ili wanaowapa wanafunzi
ujauzito au kuwakatisha masomo ili waozeshwe wapate adhabu stahiki.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
chanzo:Mpekuziblog.
Comments