WAZIRI
MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika
viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu.
Amesema
Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo
ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.
Ameyasema
hayo Jumapili, Julai 30, 2017 wakati akizungumza na wafanyakazi wa
kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe.
Waziri
Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji
nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.
“Mnatakiwa
muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa
ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.”
Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao.
Awali,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na
kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa
kuzalisha tani 46 kwa siku.
Alisema
gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa
nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.
Mhandisi
Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea
soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya
kuzimia moto.

chanzo:Mpekuziblog.
Comments