
Hayo yamesemwa na waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Julai 5, 2017
bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa saba wa
Bunge la 11. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.
“Katika kipindi kifupi tangu Februari, 2017 Mamlaka hii
ilipozinduliwa, imefanikiwa kukamata watuhumiwa 4,809 wakiwa na dawa za
kulevya aina ya heroine (gramu 327.173); cocaine (kilo 26.977); bangi
(kilo 18,334.83); mirungi (kilo 11,306.67) na lita 6,338 za kemikali
bashirifu zilikamatwa bandarini,” amesema.
Majaliwa amesema mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi za
Mikoa imefanya operesheni za kuteketeza ekari 569.25 za mashamba ya
bangi na ekari 64.5 za mashamba ya mirungi na kazi hiyo inaendelea.
Kutokana na hatua hizo, jumla ya majalada ya kesi 3,222 yamefunguliwa.
“Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa ustawi wa familia zetu na
Taifa kwa ujumla. Hivyo, napenda kurejea wito wangu kwa Watanzania wote
kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano haya kwa kuendelea
kutoa taarifa kuhusu watu wote wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya.
Amesema azma ya Serikali ya awamu ya tano ni kutokomeza kabisa
mtandao wa dawa za kulevya nchini kwa kuhakikisha kuwa mapambano dhidi
ya dawa za kulevya yanakuwa endelevu, yanafanyika kisayansi na yanaleta
mafanikio. “Tuungeni mkono kwenye mapambano haya, ili tutokomeze kabisa
mtandao huo,” amesisitiza.
chanzo:dar24.
Comments