Watoto wenye matatizo ya Miguu Rungu waongezeka Mnazi Mmoja.

mnaziWatoto wenye miguu rungu wanaopatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja imeongezeka kutoka watoto watatu kwa mwezi hadi kufikia saba.

Mratibu wa kitengo cha miguu rungu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dk. Salim Seif Ali alisema kwamba ongezeko hilo linaonesha kuwepo kwa uelewa miongoni mwa wazazi na walezi wenye watoto wenye matatizo hayo.


“Mwanzoni tulikuwa tukipokea watoto wawili, watatu, lakini tuliendelea na kutoa elimu kwa jamii na sasa kumekuwa na mafanikio, ingawa bado tunaendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi kuhusu matatizo ya miguu rungu” Alisema Dkt. Salim Seif.

Mratibu wa Klinik hiyo alisema kwamba matibabu wanayotoa kwa watoto wenye matatizo ya miguu rungu yameonesha mafanikio makubwa kwani kiasi kikubwa cha walio patiwa matibabu wamepona wameweza kurudi  katika hali za kawaida.

“ZOP wamefanikiwa kwa asilimia 98% japokuwa hakuna tathmini  kamili lakini takribani wote tulio watibu wamefanikiwa kuondokana tatizo lao la mguu rungu ” aliongeza kusema Dkt, Salim.

Hata hivyo,  alisema kuwa mguu rungu si ulemavu bali ni tatizo linalotokana na mazingira ya mama anayo ishi, lakini chanzo cha tatizo hilo hakijaweza kufahamika hadi sasa.

Ali sema tatizo hilo linatibika likiwahiwa mapema pale mara tu mama anapojifungua kuanzia siku moja hadi miaka minne kwa kutumia unga wa piopio kunyosha  mifupa ya mtoto huyo mwenye mguu rungu kwa hatua ya awali.

Dkt. Salim alisema kitengo hicho kipo mnazi mmoja kwa unguja na kinatoa matibabu bure bila malipo kwa ushirikiano wa Serikali jumuiya ya  Zanzibar Outreach Program(ZOP).

Akifahamisha kuwa kitengo hicho kinakabiliwa na upungufu wa wataalamu, na kuishauri Serikali  kuweka  katika mitaala yake ya elimu ya afya Mbweni kuingiza somo litalo kabiliana na maradhi hayo ya mguu rungu pamoja na kufungua matibabu katika hospitali za mikoa  kama vile kivunge na makunduchi kwa unguja ilikuwapunguzia safari ndefu wazazi kuifuta huduma hiyo mnazi mmoja.
 chanzo:zanzibar24.

Comments