
Hayo amesema Dkt Fadhil Mohammed Abdullah mkurugenzi wa kinga na
elimu ya afya kwa niaba ya waziri wa afya wakati alipokuwa
akikaguwa kituo cha afya kilichokuwa meli nne katika jimbo la
kijitoupele.
Amesema kituo hiki cha afya kilichojengwa hapo kina umuhimu
mkubwa sana hasa ukizingatia katika jimbo hilo linaishi watu wengi
sana hivyo kitakapokamilika na kuanza kazi kutaweza kupunguza idadi ya
wagonjwa wengi wanaokwenda katika hospitali ya Fuoni au Mnazi mmoja.
Dr Fadhil amesema wananchi katika majimbo yao wana chachu kubwa ya
kupatiwa maendeleo hivyo amewashukuru viongozi wa jimbo hilo kwa kuamua
kujenga kituo hicho.
“labda niwashukuru viongozi wa jimbo hili kwa uamuzi walioufanya kwa
kujenga kituo hiki cha afya katika eneo hili kwani kutaweza kuwaletea
faraja kubwa wananchi wa jimbo hilo,” alisema mkurugenzi huyo.
Pia amesema kituo hiki kitakapokamilika kitakuwa kinatoa huduma zote
muhimu ambazo zinatolewa katika hospital kuu ya mnazi mmoja ikiwemo
sehemu ya kujifunguliya akinamama , ushauri nasaha, chanjo kwa akinamama
na watoto, meno, na kupima presha na baadhi ya maradhi mengine.
Vile vile amewashauri wananchi hao kuwa na utaratibu wa kwenda vituo
vya afya kwenda kupima afya zao kila baada ya muda na kupata kujua afya
zao kwani kinga bora kuliko kutibu.
Nae mwakilishi wa jimbo hilo Ali Suleiman Shihata akitoa shukurani
zake kwa viongozi wa jimbo hilo wakiwemo waliopita na wa sasa hivi kwa
kukamilisha kituo hichi ikiwa ni moja ya ahadi zake alizoziahidi wakati
wa kampeni na sasa wanatimiza ahadi zao akiwemo mbunge na mwakilishi wa
jimbo hilo.
Pia mwakilishi huyo ameahidi kuwa kitakapomaliza kituo hicho
madaktari na manesi pamoja na wahudumu wengine watatoka katika jimbo
hilo ili kupunguza usumbufu wa kwenda masafa marefu.
Jumla ya million 84 na laki nne zimetolewa na viongozi wa jimbo hilo
wakiwemo mwakilishi na mbunge katika kukamilisha kituo hicho.
Nao wananchi wa jimbo hilo wametoa pongezi zao kwa viongozi wao wa
jimbo kwa kupatiwa kituo cha afya ndani ya jimbo lao na kusema kuwa
watapunguziwa kwenda masafa marefu kuifata huduma hiyo hasa akinamama na
watoto.

Picha: Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Ali Sleiman Shihata akitoa
maelezo ya ujenzi wa kituo kipya cha Afya kwa timu ya watalamu kutoka
Wizara ya Afya walipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Wa
katikati ni Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dkt. Fadhil Mohammed
Abdalla na (kulia) ni Diwani wa Kijitoupele Saleh Kinana.

Picha:Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla
akisoma ramani ya kituo hicho na kutoa maelekezo kwa mafundi wanaojenga
kituo hicho (katikati) Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Ali Sleiman
Shihata na wapili (kulia) ni Msaidizi daktari dhamana kanda Unguja Ali
Kassim Amour.

Picha:Muonekano wa jengo jipya la kituo cha Afya cha Kijitoupele
linalojengwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na
Mwakilishi Mhe. Ali Sleiman Shihata kwa kushirikiana na wananchi wao.
chanzo:zanzibar24.
Comments