Wananchi Wametakiwa kutumia bidhaa za asili Zanzibar.

Image result for newsJamii imehamasishwa  kutumia bidhaa  za asili zinazotokana  na zao la  mwani, ili kujenga afya bora kwa maisha yao.
Akizungumza na Zanzibar24 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Riziki Pembe Juma pamoja na baadhi ya wananchi  wamesema bidhaa hizo zilizotengenezwa kwa mwani  zinaubora zaidi kwani  zinatibu  magonjwa mbalimbali.

Amesema Mwani hutengezewa  Aina kumi na saba  za bidhaa ambapo ni sabuni,mafuta,loshani,saladi,chakula,pia husaidia magonjwa mbalimba  ikiwemo maradhi ya ngozi,pia hutia damu  hasa mama wajawazito  huwasaidia katika  kuwajengea afya bora watoto tokea tumboni.
Hata hivyo wamesema  kutokana na umuhimu wa zao hilo duniani  ipo haja wawekezaji pamoja na wadau mbalimbali kushirikiana na serikali  kuwasaidia  wakulima wa zao hilo ili waweze  kujipatia kipato chao na kuweza kuliinua taifa kiuchumi.
Aidha  Riziki amesema Mwani ni zao la tatu kwa  Zanzibar kuingiza fedha za kigeni lakini wakulima bado  wahajanufaika na kusema kuwa serikali ipo katika mipango ya kuwawezesha wakulima pamoja na kuangalia uwezekano wa kupandisha bei ya zao hilo angalau lifike kilo mia 600  ambalo sasa kilo 300.
chanzo:Zanzibar24

Comments