Wananchi wa kijiji cha miwani watoa malalamiko kwa serikali.

Wananchi wa kijiji cha Miwani wameiomba serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuwajengea Barabara kwa kiwango cha lami ili waweze kunufaika na huduma za usafiri kijijini hapo.

Wakizungumza na Mwanahabari wetu kwa maskitiko makubwa Baadhi ya wananchi hao wamesema mbali na kuwaomba viongozi wao wa majimbo kusimamia matengenezo ya Barabara hiyo lakini mpaka sasa hawajaona matengenezo yoyote.


Wamesema kwa muda mrefu sasa wanapewa ahadi na viongozi wa serikali pamoja na viongozi wa majimbo kuwa barabara hiyo itatengenezwa lakini hawajaona matengenezo na kulazimika kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo kijijini hapo.

Aidha wamesema kijiji hicho kinashindwa kukuwa kiuchumi kutokana na wananchi wake kushindwa kusafirisha bidhaa wanazozalisha kupeleka masokoni kutokana na ubovu wa barabara unaosababishia wamiliki wa magari kushindwa kutoa huduma ya usafiri kwa uhakika.

Zaidi ya miaka kumi wananchi wa miwani wamekuwa wakilalamika tatizo la ubovu wa barabara bila ya kupatiwa ufumbuzi na kuwasababishia wananchi matatizo ikiwemo wajawazito kujifungulia njia.
chanzo:Zanzibar24.

Comments