Jumla ya wananchi elfu kumi [10,000] wanatarajiwa kufaidika na mradi wa
umeme kutoka ukujwi hadi fundo mara utakapokamilika mwishoni mwa mwezi
huu.
Mradi huo ambao utagharimu jumla ya billioni mbili hadi kukamilika kwakwe unafadhiliwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kutokana na mapato yake ya ndani katika jitihada za kuwapatia wananchi wake huduma muhimu za kijamii .
Akitoa maelezo mara baada ya kutembelea maeneo ya mradi huo kujionea hatua uliofikia katibu mkuu wizara ya ardhi maji nishati na mazingira nd alhalili mirza amesema huduma hiyo itasaidia kubadilisha maisha ya wananchi katika nyanja mbali mbali kama vile uchumi na maendeleo kwa kujishughulisha na biashara ndogo ndogo elimu na mambo mengine.
Kwa upande wake kaimu meneja wa shirika la umeme Pemba nd mohd juma othman amesema mradi huo umefikia katika hatua za mwisho za utekelezaji wake na wakati wowote ndani ya mwezi wa saba utakamilika na kuwanufaisha wananchi.
Kukamilika kwa mradi huo ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi za rais wa zanzibar dr ali mohd shein alioitoa mwaka huu wakati akifungua ofisi ya baraza la mji na soko la wete huko mkoa wa kaskazini Pemba.
chanzo:Zbc.
Comments