WANACHAMA WA ZSSF KUNUFAIKA NA MKOPO WA ELIMU.

Wanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii zanzibar zssf wanatarajiwa kunufaika na fursa za kielimu baada ya mfuko huo kuamua kuwakopesha wanachama wake katika kuongeza taaluma.

Kaimu mkurugenzi  wa mfuko huo makame mwadini silima akizungumza wakati wakisaini makubaliano baina ya mfuko huo na benki ya posta tanzania amesema pamoja na fursa hiyo ya kielimu makubaliano hayo pia yanahusu mkopo kwa wanachama wa zssf wanaoanza maisha.


Amesema mfuko umelenga kuwanufaisha wanachama katika nyanja mbalimbali huku akiahidi kutolewa elimu ili kuwafahamisha jinsi ya kutumia fursa hiyo pamoja na masharti yanayohitajika ili kupata mikopo hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa benki ya posta tanzania sabasaba mushingi amesema benki inakusudia kutatua changamoto hasa kwa vijana wanaoanza maisha baada ya kuajiriwa kwa kukosa huduma muhimu kutokana na kutokuwa na fedha za kujiandaa na maisha.

Mkopo wa elimu utakaotolewa kwa wanachama wa mfuko huo ni kwa viwango mbalimbali ikiwemo cheti hadi phd katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.
 chanzo:Zbc.

Comments