Wafanyakazi kujiendeleza kitaalam ili kuweza kuendana na kasi ya mabadiliko ya shirika la utangazaji zanzibar.

Waziri wa habari utalii utamaduni na michezo mh rashid ali juma amesema ipo haja ya wafanyakazi kujiendeleza kitaalam ili kuweza kuendana na kasi ya mabadiliko ya shirika la utangazaji zanzibar.

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo amesisitiza matengenezo yanayoendelea katika shirika hilo litaendana nauwepo wa vyombo vipya vya kisasa hivyo ni vyema kujitayarisha ili kukabiliana navyo na kuacha kufanyakazi kimazowea.


Amefahamisha kuwa ushirikiano uliopo baina ya uongozi na wafanyakazi wa shirika hilo unawezesha kufanyika kazi kwa uhakika hivyo ni vyema kupeana kupeana motisha za kimasomo ili kujijenga.

Mshauri wa waziri wa habari mh abdalla mwinyi amesisitiza viongozi kutumia hikima katika maamuzi wakiwa kazini ili kuwawezesha wafanyakazi kuwajengea mazingira mazuri katika sehemu zao za kazi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika imane duwe hilo amesema wafanyakazi wa shirika hilo ni wenye kukubali mabadiliko hivyo hana wasiwasi na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi katika kasi ya mabadiliko.

chanzo:Zbc.

Comments