
Walisema hayo
wakati wa kikao cha kujadili mfumo nzima wa kuanzisha mfuko wa
kujisomeshea kwa waandishi wa habari waliopo kisiwani Pemba,
unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Walisema kuwa,
ili kuendeleza umoja huo na kuona tasnia ya habari inasonga mbele zaidi,
ni vyema kwa waandishi hao kuacha tofauti zao na kuacha ubaguzi, jambo
ambalo, litaweza kuwasaidia katika kuimarisha maendeleo ya habari.
Mkutano huo wa
kuanzisha mfuko wa kujisomeshea kwa waandishi wa habari Pemba,
ulifanyika katika ukumbi wa Jumuiya ya waandishi wa habari Pemba (PPC),
ukiwa na lengo la kumuwezesha mwandishi kupata fedha zitakazomsaidia
kujiendeleza na masomo.
Mmoja wa
waandishi walihudhuria kikao hicho kutoka kituo cha redio Istiqama Salim
Ali Msellem alisema kuwa, kuanzishwa kwa mfuko huo, utawafanya
wanahabari kuwa wamoja na sio kufarikiana.
“Popote kwenye
kheri na bilisi hutembelea, hivyo ni vyema tukaweka uaminifu katika
mfuko wetu wa fedha, ili tuweze kujiendeleza kielimu”, alisema mwandishi
huyo.
Kwa upande wake
mwandishi Abdi Suleiman kutoka shirika la magazeti ya Serikali kisiwani
humo, alileza kuwa, mfuko huo wa fedha wa kuwawezesha kujisomeshea, iwe
ni chachu ya maendeleo na uweze kuzaa matunda, ili kuwanufaisha
waandishi kisiwani Pemba.
Nae mwandishi na
mpiga picha wa shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC), Raya Ahmada Mohamed
alisema kuwa, kuanzishwa kwa mfuko huo ni faraja kubwa kwao, kwani
utawawezesha kuwasaidia waandishi wasio na uwezo wa kujiendeleza na
elimu ya juu.
“Kwa kweli wengi
wetu tunashindwa kujiendeleza kielimu kutokana na kukosa fedha za
kujisomeshea, lakini tutakapoanzisha mfuko huu, tutajikwamua na hali
hii”, alieleza Raya.
Mapema
Mwenyekiti wa muda wa Mfuko huo huo Haji Nassor Mohamed alisema kuwa,
lengo la kuanzishwa kwa mfuko wa kujisomeshea kwa waandishi wa habari,
ni kumrahisishia mwandishi kujiendeleza kielimu, bila ya usumbufu pamoja
na kuipeleka mbele tasnia ya habari.
“Mfuko huu ni
muhimu sana kwetu, iwapo tutakuwa tayari kujitolea kwa kuanzishwa kwake,
tunaweza kusonga mbele katika kujiendeleza na masomo ya ngazi za juu”,
alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha aliwataka
waandishi hao, kuwa na msimamo madhubuti sambamba na kuwa waaminifu
katika mfuko huo, ili kuweza kuwanufaisha wao na taifa kwa ujumla.
Akzungumza kwa
njia simu, mshauri wa mfuko huo Ali Hji Hamad, alisema dhana hiyo ni
mzuri na inafaa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ya kielimu na
wanahabari kwa ujumla.
“Mfukp mzuri hasa
kwa hilo lengo kuu la kuwasomeshea waandishi, maana wapo walio na hamu
ya kusonga mbele lakini wanakwaza na fedha za kujiendeleza hivyo jengeni
moyo wa ujasiri na uaminifu”,alishauri.
Mfuko wa
kuwaendeleza kielimu waandishi wa habari kwa kuwapatia fedha taslimu
kisiwani Pemba, unaweza kuwa mwanzo Tanzania hasa katika siku za hivi
karibuni, ambapo zaidi ya waandishi 30 wanatarajiwa kuwa wanachama,
ambao watachangia kati ya shilingi 30,000 hadi shilingi 50,000 na
wastani wa shilingi 1.5 milioni zinatarajiwa kukusanywa.
chanzo:zanzibar24.
Comments