Viumbe vya bahari hatari kutokana mufuta kusambaa baharini Wesha Kusini Pemba.

Kiasi ya lita 200 za mafuta ya IDO zilizomwagika  kutoka katika meli ya LCT RAHIMA  na kuenea katika gati ya bandari ya Wesha HUENDA zikahatarisha maisha ya viumbe vya bahari na miti iliyozunguka bandari hiyo.

Akizungumza na mwandishi wetu  Mkuu wa Idara ya mazingira Pemba Mwalimu Khamis Mwalimu amesema mafuta hayo yameenea katika eneo lenye ukubwa wa mita 200 hali ambayo inaweza kusababisha uchafuzi wa mazingira na kupoteza maisha ya viumbe vya baharini.


Amesema kwa hatua ya awali kuna watu wameanza kuyafyoza mafuta hayo kwa kutumia masponji ili kuepusha athari zaidi na kulinda mazingira ya eneo hilo.

Akielezea chanzo cha kumwagika mafuta hayo nahodha wa meli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la MALBORO amesema meli hiyo ilifika salama kutoka bandari ya Wete na taratibu zote za ukaguzi zifanyika laki mara baada ya maji kutoka meli ili jigonga na jiwe na kuanza kumwaga mafuta.


Msimamizi wa bandari ya Wesha BIBI Moza Moh’d Amour amesema hii ni bahati mbaya na mara ya kwanza meli kuvujisha mafuta na kwa sasa ni mamlaka ya bandari na mazingira kukaa pamoja na kutafuta njia ya kuyaondoa mafuta hayo ili kuepusha hali kuwa mbaya zaidi.

Comments