VIONGOZI WA MAJIMBO WAMESHAURIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO ILI KUFANIKISHA AHADI ZA VIONGOZI WAKUU.

Viongozi wa majimbo wameshauriwa kutekeleza majukumu yake ili kusaidia kufanikisha ahadi za viongozi wakuu wa serikali.

Mwakilishi wa jimbo uzini mohamed raza amesema viongozi hao wakiwemo wabunge wawakilishi wanawezeshwa na serikali kwa lengo la kufanikisha kazi za kusaidia maendeleo ya wananchi.


Akizungumza kuhusu maendeleo ya utendaji wa kazi za serikali za jamhuri ya muungano wa tanzania amefahamisha kuwa kumekuwa na mafanikio ya kazi ambayo yamejenga imani kwa wananchi.

Hivyo mh. Raza amewaomba watendaji wa taasisi kubadilika kwani taifa halihitaji mtu au kiongozi kuharibu mafanikio yaliyopatikana kwa makusudi.
chanzo: zbc.

Comments