Mkurugenzi idara ya uratibu tawala za mikoa na serikali za mitaa, nd. Khalid abdalla omar, amesema mfumo huo wa kuwashirikisha wananchi utawapa fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na utekelezaji sheria na mipango iliyowekwa kwa ajili ya shughuli za kijamii.
Akizungumza na viongozi wa dini, watendaji wa serikali za mitaa na watu wenye ushawishi katika jamii, wakati wa mafunzo ya ushirikishwaji wa wananchi katika utayarishaji wa katiba na sheria, amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa serikali inasimaia na kuimarisha utawala bora kwa wananchi wake.
Wakitoa mafunzo hayo maafisa mipango kutoka kituo cha huduma za sheria zanzibar, nd. Thabit abdalla na ali haji hassan, wameelezea majukumu ya viongozi katika kushirikiana na jamii katika shughuli za kimaendeleo.
Washiriki hao kutoka mkoa mjini magharibi wameelzea umuhimu wa viongozi kuzingatia maadili katika kazi zao.
chanzo:Zbc.
Comments