Umuhimu wa kutoa elimu kwa wanandoa watarajiwa ili kuepuka migogoro katika ndoa.

Naibu waziri wa nchi afisi ya makamu wa pili wa rais mh: mihayo juma nunga amesema upo umuhimu wa kutoa elimu sahihi kwa wanandoa watarajiwa ili kuepuka migogoro na talaka katika ndoa

Akizungumza katika mkutano na mashekhe na wanazuoni kuhusu athari athati za talaka ,migogoro ya ndoa kwa maendeleo ya ya familia Mhe: Mihayo amesema kuongozeka kwa migoro ya ndoa na talaka kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii kutokuwa na mwamko wa kupata taaluma ya kisheria ya dini hivyo ipo haja kwa jamii kuwa tayari kupeana taaluma ya ndoa kabla ya kuona.

Wakielezea mada ya usahihi wa ualii na migogoro ya ndoa na talaka katika familia ,masheikh kutoka afisi ya mufti ya zanzibar shekh thabit nuuman jongo na ustadhi khamis gharib khamis wameeleza kuwa ili kuepusha migogoro na talaka kwa wanandoa ni lazima ni lazima walii kufanya uchunguzi kwa familia za wanandoa watarajiwa na kujiridhisha na uchunguzi huo kupitia vigezo vyake mtume muhammad s.a.w.


Baadhi ya washiriki wamesema taaluma potofu kwa wanandoa kunachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko hilo hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kuweza kupunguza tatizo hilo.

chanzo:Zbc.

Comments