UJUMBE WA WATU 10 KUTOKA SERIKALI YA MJI WA ZHONGLOU KATIKA JIMBO LA CHANGZHOU NCHINI CHINA UMEFANYA MAZUNGUMZO.
Waziri wa Biashara, Viwanda na masoko Balozi amina salum ali ambae
alikuwa mwenyeji wa mkutano huo ameuambia ujumbe huo kuwa zanzibar
imetenga eneo kubwa la kuwekeza hivyo ameuomba uongozi huo kuangalia
maeneo gani ambayo wanaweza kushirikiana na zanzibar kwa manufaa ya
pande mbili.
Amesema sekta ya afya pia inahitaji ushirikiano kama ilivyofanywa kwa
Hospitali ya Abdalla mzee ambapo serikali ya china imetoa msaada mkubwa
katika kuiimarisha.
Naibu Meya wa mji wa Zhonglu Han Jun ameahidi kuwa watashirikiana
katika nyanja mbalimbali ili kukuza uhusiano kati ya china na Zanzibar
katika kukuza maendeleo.
Mkutano huo umehusisha karibu wizara tisa za Serikali Ya Mapinduzi
Zanzibar, pamoja na taasisi na taasisi zake ikiwemo mamlaka ya vitenga
uchumi zipa.
chanzo:Zbc.
Comments