
Ufadhili huo wa Watanzania 96 ni kutoka Serikalini, sekta
binafsi na asasi za kiraia, wamenufaika kimasomo kutoka seriklai ya
Uholanzi ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali hiyo kuchangia maendeleo
nchini.
Akiongea katika ghafla fupi ya kuwaaga Watanzania hao,
iliyofanyika katika ukumbi wa Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam,
Balonzi wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe. Jaap Frederiks alisema kwamba
Serikali ya Uholanzi kwa muda mrefu imekuwa ikichangia miradi ya
maendeleo nchini Tanzania.
Balozi Jaap alieleza kuwa Watanzania waliofaidika na mpango
huo unaojulikana kama Netherlands Fellowship Programme – NFP, ni
waajiriwa kutoka Serikalini, sekta binafsi, wafanyabiashara wadogo
pamoja na waajiriwa kutoka Asasi za kirai.
“Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa moja kati ya wafaidika
wakubwa wa ufadhili wa Masomo Nchini Uholanzi program inayojulikana kama
“Netherlands Fellowship Programme – NFP” ambapo zaidi ya Watanzania
5000 wamefaidika na ufadhili huo katika kozi mbalimbali”. alisema Mhe.
Balozi Jaap.
Serikali ya Uholanzi imekuwa ikitoa mafunzo ya kuwajengea
uwezo baadhi ya Watanzania pamoja na kuboresha Sekta ya rasilimali watu,
tukiamini kwamba kupitia watu hao tunachangia katika maendeleo ya
Taifa.
Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma
katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya
hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi nchini
humo.
chanzo:zanzibar24.
Comments