Tundu Lissu Azungumzia Sakata la Madiwani wa CHADEMA Kuhamia CCM........Pia Kazitaja Sababu za CHADEMA Kuingilia Mgogoro wa CUF .
Mbunge
wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS),
Tundu Lissu amesema Ukawa unatangaza vita na CUF ya Profesa Ibrahim
Lipumba kama walivyo vitani na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lissu
ameyasema hayo jana wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari katika
makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni, Jijini Dar es salaam.
Alisema kwa kuwa chama hicho ni miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA, watahakikisha wanaingia vitani kumong’oa Prof. Ibrahim Lipumba aliyedai kuwa ni msaliti
Alisema kwa kuwa chama hicho ni miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA, watahakikisha wanaingia vitani kumong’oa Prof. Ibrahim Lipumba aliyedai kuwa ni msaliti
“Profesa
Lipumba ametusaliti kwa kuwa yeye ndiye aliyempitisha Lowassa kuwa
mgombea wa urais kwa tiketi ya Ukawa. CUF ya Lipumba ilitusaliti kama
Yuda Iskarioti alivyomsaliti Yesu Kristo,” alisema Lissu.
Mgogoro
wa CHADEMA na CUF ya Lipumba ulianza baada ya kiongozi huyo kuandika
barua ya kujiuzulu Uenyekiti wa chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu
mwaka 2015 na baadaye kutaka kurejea katika nafasi yake hali
iliyosababisha mpasuko ndani ya Ukawa pamoja na CUF kwa ujumla.
Akizungumzia
kuhusu kitendo cha baadhi ya madiwani na wenyeviti wa chama hicho
kuhamia CCM kutokana na hali ya kuridhishwa na uchapakazi wa Rais John
Magufuli, Tundu Lissu aliwavaa viongozi hao na kuwatuhumu kuwa
wamekiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1997 na kwamba
wamekiuka viapo vya maadili kwa sababu kuhama kwao kumesukumwa na
rushwa.
Alidai kwamba, mmoja wa viongozi hao ambaye hakumtaja jina, wiki moja baada ya kuhamia CCM aliteuliwa kuwa Mchumi wa Halmashauri ya Arumeru, jambo ambalo amelifananisha na kula rushwa.
Alidai kwamba, mmoja wa viongozi hao ambaye hakumtaja jina, wiki moja baada ya kuhamia CCM aliteuliwa kuwa Mchumi wa Halmashauri ya Arumeru, jambo ambalo amelifananisha na kula rushwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments