TRL Yavikataa vichwa vya treni Vilivyo Bandarini.......TPA Wanadai ni Vyao ila tu Kuna Mgogoro Ambao wao Hawakutaarifiwa.
Kampuni
ya Reli Tanzania (TRL) imekanusha kuhusika na vichwa 11 vilivyoshushwa
na kutelekezwa katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), Deusdedit Kakoko, vichwa hivyo vilivyoshushwa na meli ya Mesina
Line tangu wiki iliyopita, na kwamba ni mali ya TRL.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni hiyo, Masanja Kadogosa jana alisema TRL haihusiki kwa
namna yoyote na vichwa hivyo kwa kuwa hakuna taarifa zozote zinahusu
uagizwaji wake.
Alisema
pia kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi, kampuni hiyo inapofanya manunuzi
yoyote lazima kuwepo na mkataba wa makubaliano na kampuni husika
inayouza bidhaa, lakini haina mkataba wowote unaohusu ununuzi wa vichwa
hivyo.
Alieleza
kuwa taratibu za manunuzi zinafahamika kwani endapo kampuni hiyo
ingeagiza vichwa hivyo ingetakiwa kupeleka mtu wake kwa ajili ya ukaguzi
wakati vinatengenezwa na mara baada ya kutengenezwa kabla ya kupakiwa
kwenye meli. “Lakini hiyo kitu hakuna, hatukuwa na watu wetu kwa kuwa si
mali yetu,” alieleza.
Pamoja
na hayo, alisema ili mzigo wowote umfikie mhusika lazima kuwepo na
nyaraka ya kutolea mzigo bandarini ambayo pia huwa na makubaliano
mengine baina ya mnunuzi na muuzaji ambayo katika sakata hilo, TRL
wamesisitiza hawana nyaraka hiyo.
Alisema
TRL haivitambui vichwa hivyo kwa kuwa si mali yake. “Hivi ni vichwa
vikubwa sasa kwanini tuvikatae kama ni vyetu, ila ukweli ni kwamba
hatuvitambui kabisa,” alieleza mkuu huyo wa reli nchini.
Juzi
wakati akizundua Mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam
(DSMGP), Rais John Magufuli aliibua hoja hiyo ya vichwa vya treni
kushushwa bandarini na kutekelezwa bila kuwa na mwenyewe na kuitaka TPA
pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kufuatilia kwa kina
suala hilo.
Dk
Magufuli alisema anazo taarifa za kushushwa kwa vichwa vya treni
takribani 15 katika bandari hiyo, ambavyo mmiliki wake hafahamiki na
meli iliyovileta imeshaondoka.
Hata
hivyo, mkurugenzi wa mamlaka hiyo ya TPA Kakoko pamoja na kuthibitisha
kushushwa kwa vichwa hivyo kutoka kwa meli ya Mesina Line, iliyobeba
mzigo huo kutoka kwa Komazi Trading Co, alibainisha wazi kuwa vichwa
hivyo ni vya TRL.
Alisema
vichwa hivyo ni awamu ya pili iliyoagizwa tangu serikali ya awamu ya
nne miaka mitatu iliyopita, ambapo awamu ya kwanza ilishaletwa na vichwa
vyake kuchukuliwa na hadi leo vinatumiwa na TRL.
Alifafanua
kuwa baada ya uchunguzi wa TPA ilibaini kuwa kuna mgogoro unaoendelea
kati ya TRL na kampuni ya Komazi na kwamba TRL ilishagoma kuvichukua
vichwa hivyo lakini suala hilo, halikutaarifiwa kwa TPA
chanzo:Mpekuziblog.
Comments