
Akizungumza na Mwandishi wetu Katibu wa Sheha wa shehia ya Kilombero
John Ndarami Makeja amesema kukosekana kwa huduma ya maji safi na
salama kunawapa wasiwasi mkubwa kupata ugonjwa wa Mripuko kutokana na
wananchi walio wengi kutumia maji ambayo hayapo salama kwa
kunywa,kupikia pamoja na kufanyia shughuli nyengine kwa mahitaji ya
nyumbani.
Kwaupande wake Afisa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa Zahor Suleiman
Khatib amesema kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama katika
shehia ya kilombero kuna sababishwa na ubovu wa mashine pamoja na pampu
yakupelekea maji katika mabomba.
Hata hivyo Zahor ametoa wito kwa wananchi wa kilombero kuwacha
kutumia maji ya mito na visima visivyo na usalama na badala yake kwenda
kuchota maji katika maeneo jirani ili kunusuru wananchi kuugua ugonjwa
wa kipindupindu wakati huku mamlaka inaendelea na jitihada za
kuitengeneza mashine hiyo ili kurudisha huduma ya maji katika maeneo
yao kama awali.
Nae Mwakilishi wa Jimbo hilo la Kiwengwa Asha Abdalla Mussa amewataka
wananchi wa kilombero kuwa na subra kwani viongozi wa jimbo kwa
kushirikiana na Mamlaka ya Maji zawa wanalitafutia ufumbuzi tatizo
hilo linalowakabili.
Hivi karibuni Vijiji cha Kilombero kilikubwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na matumizi ya maji yasio salama kiafya.
chanzo: zanzibar24.
Comments