
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya
matajiri waliowahi kukamiliwa na janga hilo la utapeli kwa kukodishwa
mashamba yaliyokodishwa kwa watu zaidi ya mmoja.
Walisema mtu anaetaka kukodi shamba la
mikarafuu, ahakikishe wamiliki wa pembe nne za shamba yanayo mzunguka
wanakuwepo, ili kukwepa migogoro ya makusudi wakati wa kuvuna zao hilo.
Hamad Ali Ramadhan wa Wete alisema,
alikodishwa shamba eneo la Kigope Mkoani, wakati shamba hilo tayari
lilishakodiwa na mkwe wake, wiki tatu zilizopita.
“Mkwe wangu alikodi shamba
hilo kwa shilingi milioni 8, (8,000,000) na kisha kuwakabidhi watu na
yeye kurudi anakoishi Nairobi Kenya, lakini juzi nusura likodishwe tena
mara mbili”,alifafanua.
Aidha Hassan Haji Vuai wa mjini
Chakechake, alisema alikodi shamba maeneo ya Ngomeni, siku ya kukabidhi
fedha, ndipo alipotokezea mtu waliepakana na hatimae mikarafuu 10,
ilishakodishwa wakati sio halali kwa mwenye shamba.
“Baada ya kuona hivyo alitaka
kunikodisha ugomvi, niliamua kurejea na fedha zangu shilingi milioni
5,000,000 na kwenda Mgelema na huko nimeshakodi shamba chini ya wamiliki
wa wote wanne waliolizunguruka shamba hilo.
Kwa upande wake, sheha wa shehia ya
Mgelema Omar Iddi Zaina, aliwatahadharisha wananchi wanaotaka kukodi
mashamba hasa ndani ya shehia yake, wasikubali kufanya hivyo, pasi na
kuwepo uongozi wa shehia.
“Kama wakihisi sheha
hawamuhitaji, basi kabla ya kukodi wawapate waliopakana na shamba
wanalotaka kulikodi, ili kuepusha utapeli unaoweza kufanywa”,alifafanua.
Maeneo ambayo tayari kumesharipotiwa
ukiukwaji wa mipaka au shamba moja kukodishwa zaidi ya mara moja ni
pamoja na Mtambile, Jungani, Mkanyageni, Wambaa, Mgelema, Ngomeni na
Ziwani.
chanzo: zanzibar24.
Comments