Taasisi yapiga jeki shughuli uhifadhi pori la Lukwati.

Askari wanyapori waliopatiwa mafunzo kutokana
Taasisi ya Kimataifa ya kijamii ya uhifadhi wa wanyamapori ya World Conservation Society (WCS) imetoa msaada wa zaidi ya Sh936 milioni kwa mapori ya akiba ya Lukwati-Piti ambazo zimetumika kujenga jengo la kisasa la ofisi, ununuzi wa magari matatu ya doria na kuendesha mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa mapori hayo yaliyoko mkoani Songwe.
Akiongea katika halfa ya kukabidhi miradi hiyo kwa serikali, Mkurugenzi wa WCS, Aaron Nicholaus, amesema taaisisi hiyo inajivunia kushirikiana na serikali ya Tanzania kuendeleza uhifadhi wa wanayamapori wakiwemo tembo ambao ni maliasili muhimu kitaifa na kimataifa.

Nicholaus amesema msaada huo umetilia mkazo suala la mafuzo ambayo yatawaongezea askari ujuzi na weledi wa kukabiliana na majangili ambao wamekuwa wakiua tembo na wanyamapori wengine kwa maslahi yao binafsi na kusababisha hasara kwa serikali ambayo inawategemea wanyamapori kwa maendeleo ya jamii na taifa.
“Tunapofikiria uhifadhi, tuangalie pia masuala ya mapito ya wanyamapori kama tembo ambayo yamekuwa yakitoweka kutokana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu na hivyo kuathiri uhifadhi maana tembo huhitaji eneo kubwa kwa malisho,” amesema.
Taarifa ya miradi hiyo iliyotolewa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ilieleza kuwa miradi hiyo ina thamani kubwa kwa uhifadhi wa mapori hayo yenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 6,119 ambayo yanapakana na Hifadhi ya taifa ya Ruaha na pori la akiba la Rungwa
Meneja wa Mapori ya Lukwati Piti Bwana Alphonce Ambroce Mung’ong’o akitoa ufafanuzo na mchanganuo wa gharama za miradi hiyo alisema jengo la kisasa la ofisi limegharimu zaidi ya shilingi milioni 227, magari matatu kwaajili ya doria yana thamni ya dola 255,000 za kimarekani boti na mfumo wa radio call una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 234.
chanzo:Mwananchi

Comments