Soko kuu nchini Zambia limeteketea kwa moto na kuharibu tegemeo la
wafanyabiashara wengi.Soko hilo la City Market lililo mjini Lusaka
limekuwa likiteketea tangu mapema leo Jumanne.
Kwa upande wa msemaji wa polisi Esther Katongo na meya wa mji wa
Lusaka Wilson Kalumba wanasema kuwa bado wanachunguza chanzo cha moto
huo.
Wafanybiashara wengi wamefikwa na majonzi makubwa baada kupoteza mali
yao.”Nitailisha vipi familia yangu kwa sabaua ninategemea hapa,”
alisema Loveness Banda huku akiangalia kutoka mbali soko likiteketea.
Miongoni mwa walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa moto huo
ulisababishwa na hitilafu ya umeme na kuwalaumu wazima moto kwa
kuchelewa kufika kuzuia moto huo kusambaa.
Soko hilo lina wafanyabiashara wengi zaidi nchini Zambia. Kati ya
bidhaa zinazouuzwa ni pomoja na nguo za mitumba, vifaa vya elektroniki
na hata vyakula.
chanzo:zanzibar24.
Comments