
Alisema njia hiyo ikiwemo misaada ya Kibinaadamu, vifaa pamoja na
Taaluma zinaweza kuwa chachu ya kuwaondoshea fikra potofu za kujihisi
kwamba wanatengwa na Jamii iliyowazunguuka.
Bibi Mwanaidi Mohamed alisema hayo kwa niaba ya Wawakilishi wenzake
wa Taasisi za Kijamii wakati akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa
Vifaa pamoja na vyakula mbali mbali vilivyotolewa msaada na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Kama Kaskazini
Magharibi ya Mji wa Zanzibar.
Msaada huo wa Vifaa na Vyakula ikiwa ni utaratibu wa mara kwa mara wa
kusaidia Makundi Maalum Nchini ni pamoja na Tende, Mchele, Unga wa
ngano, Mafuta ya Kupikia, Sukari pamoja na Misahafu.
Bibi Mwanaidi alisema mahitaji ya Makundi maalum yanapaswa kuangaliwa
mara kwa mara badala ya tabia ya baadhi ya watu wenye uwezo kuzingatia
zaidi utoaji wa misaada yao wakati wa vipindi vya Siku kuu.
Mapema Naibu Katibu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bibi Fatma
Abdulrahman Khatib alisema msaada huo wa vitu na vyakula umeelekezwa
kwa watoto wanaolelewa kwenye Nyumba za Mayatima za Mombasa {SOS},
Mazizini pamoja na Wazee wa Sebleni na Welezo.
Bibi Fatma alisema msaada huo ulioelekezwa pia kwa Watu wanaoishi
katika Nyumba za kurekebishia tabia { Sober House } umelenga kutoa
huduma kwa Jamii ili iweze kujikidhi Kimaisha.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
![]() |
![]() |
chanzo:zanzibar24.
Comments