SMZ yajipanga kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar  imejipanga kikamilifu kwa kuchukua hatua ya kuweza kutafuta njia mbadala ya kukimbiza vitendo vya uhalifu kutoweka nchini.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Mjini Ayoub Mohammed Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake Vuga Mjini Unguja.


Amesema hivi karibuni amefanya safari ya kuenda nchini Marekani ndani ya kampuni inayodhibiti vitendo vya uhalifu duniani kwalengo la kuagiza vifaa madhubuti vya uchunguzi yaani CCTV Camera kwa dhumuni la kufikishwa nchini ili kuchungunguza matukio mbalimbali yanayofanyika hapa nchini.

”Matumaini yaliopo mwezi ujao mwezi ujao vifaa vitaanza kufanya kazi nchini”amesema Mh Ayoub.

Amesema kufuatia tukio lililo fanyika Daraja bovu Konda wa daladala kupigwa mapanga kamati kamati maalumu ilijipanga kikamilifu kuwatafuta wahalifu wa tukio hilo, tayari wamesha tiwa mikonononi mwa Serikali ambao kwa idadi ni 44.

Hata hivyo Mh Ayoub ametoa indhari watu 336 waliobainika kuwa na tabia ya vitendo vya uhalifu kufika vituoni wenyewe ndani ya wiki mbili kuanzia Julai 30 kabla ya Serikali kuchukua hatua mikononni mmwake.

“Wazazi wa watoto wanajihusisha na vuitendo vya uhalifu kufikisha taarifa kwenye vyombo vya sheria zawatoto wao la si hivyo tutawakamata pamoja na watoto wao.”

Vile vile ametoa wito kwa wananchi kuwa kutokuwa na hofu ndani ya mkoa wao kwani upo salama na waendelee kutoa taarifa ambapo tu tatizo linapotokezea.

Ayoub ameviomba vikosi vya usalama nchini kuwa linapotokezea tukio lolote ni wajibu kulifuatilia kwa haraka zaidi kwa wakati unaofaa.
chanzo: zanzibar24.

Comments