Hayo yameelewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikowa na Idara Maalum Zanzibar Mh. Haji Omar Kheri wakati akikabidhi boti
mbili na mashine zake kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar
Dr Ali Mohd Shein kwa ajili ya kuondoa tatizo la ushafiri baina ya Kisiwa Panza
na Chokocho Kisiwani Pemba.
Amesema mpango wa Serekali nikuhakikisha tatizo la
usafiri katika visiwa vidogo vidogo vya unguja na pemba linamalizika kwa
kupatiwa boti za kisasa kwa ajili ya kuuvuushiya.
Mh. Haji amefahamisha kuwa boti hizo zitatowa huduma
bure kwa wananchi wa kijiji cha Chokocho - Kisiwa Panza na wananchi watatakiwa
kidogo kwa ajili ya gharama za mafuta ambapo wiki moja kuanzia leo itakua ni
bure.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanajuma Majid Abdallah
amepongeza juhudi za Serekali chini ya uwongozi wa Dr. Shein za kutatua kero za
wananchi katika suala zima la usafiri walioko katika Visiwa na kuwataka wananchi kuzitumia boti hizo bila ya ubaguzi.
Comments