Skauti yateua makamishna 112 watakaofanya kazi mikoa 19.

Chama cha Skauti Tanzania kimefanya uteuzi wa makamishna na naibu makamishna 112 ambao wamepangiwa kazi katika mikoa 19.
Kamishna Mkuu wa chama hicho, Abdulkarim Shah amesema uteuzi huo umefanyika leo (Julai 5) kutokana na kuwepo mikoa mipya, baadhi ya makamishna kuhamishwa kikazi na wengine kufariki dunia.
Shah amesema wameanza na mikoa ya Tanzania Bara na baadaye watafanya uteuzi wa makamishna na naibu makamishna kwa mikoa ya Zanzibar.
Amesema wateule hao ni kwa mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Mtwara, Njombe, Pwani, Lindi, Mara, Morogoro, Shinyanga, Simiyu, Singida, Tanga, Mbeya na Rukwa.
chanzo:Mwananchi.

Comments