
Miongoni mwa Vipengele vya makubaliano hayo ni kuijenga miundombinu
ya Majumba ya Mjerumani Kikwajuni ili kuhakikisha muonekano wake
inafanana na Mji wa Drewits wa Potsdam Ujerumani.
Akizungumza katika Hafla hiyo Meya wa Jiji la Potsdam Jann Jakobs
amesema amefurahi kuona mambo mbalimbali yameanza kutekelezwa kabla ya
utiaji saini jambo ambalo linaonesha matumaini mazuri.
Miongoni mwa mambo ambayo yameanza kutekelezwa ni pamoja na upandaji
Miti inayozunguka Uwanja wa Mnazi mmoja na Mtaro wa kutirishia Maji
machafu katika eneo hilo.
Meya huyo amesema atahakikisha mradi huo unafikia malengo yake kwa
ajili ya maslahi mapana ya Watu wa Ujerumani na Zanzibar kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwandishi wa mradi huo Idrissa Haji Ali amesema ili
kuufanikisha mradi huo kutakuwa na ujenzi wa mambo mbali mbali ikiwemo
Maduka, Viwanja vya kuchezea, Taa za Barabarani na barabara ili
uendanane na Mji wa Drewits.
Amesema yeye kwa kushirkiana na Wenzake walienda Ujerumani kutembelea
na kujifunza mambo mbali mbali hasa ya kimiundombinu na mazingira ili
iwe rahisi ya kutekeleza mradi huo.
Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Kikwajuni Juu, Juma Saadat Haji
amemshukuru Meya wa Mji huo pamoja na ugeni wake kwa namna
walivyojitolea kuufanikisha mradi huo wenye maslahi makubwa katika
shehia yake.
Amesema kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha wananchi wa Shehia
yake kuishi maisha mazuri ambapo huduma za kijamii zitapatikana kwa
kiwango cha hali ya juu.

chanzo: zanzibar24.
Comments