Serikali
imesema kuwa kuanzia mwaka huu wa fedha itapunguza gharama za malipo ya
awali ya thamani ya ardhi iliyopimwa kutoka asilimia 7.5 mpaka asilimia
2.5
Hayo
yalisemwa jana bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati akitoa hoja ya kuahirisha
mkutano wa bunge la 11.
Alisema
Serikali itahakikisha kuwa kila kipande cha ardhi ya Tanzania kinapimwa
ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
“Serikali
inaendelea kupunguza gharama za umilikaji wa ardhi nchini na katika
mwaka wa fedha 2017/2018, imepunguza tozo ya awali ya ardhi iliyopimwa
(premium) kutoka asilimia 7.5 ya thamani ya ardhi hadi asilimia 2.5 tu.
Natoa wito kwa wananchi kuchangamkia punguzo hili na kujitokeza kupimiwa
na kumilikishwa ardhi,” alisema Majaliwa
Hata
hivyo, aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha Ofisi za Ardhi za
Kanda kwa kupeleka wataalam wa kada mbalimbali na kuwawezesha kwa
kuwapatia vitendea kazi stahiki
chanzo:Mpekuziblog.
Comments