Serikali inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa maji.

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa maji unaolenga kumaliza tatizo la maji katika maeneo ya mji wa zanzibar.

Mradi huo unagharimu zaidi ya dola milioni tisini na mbili ikiwa mkopo wa gharama nafuu kutoka serikali ya india unakusudia kutatua kero ya huduma ya maji katika mkoa wa mjini magharibi.


Waziri wa ardhi maji nishati na mazingira mh: salama aboud talib akizungumza na balozi wa india nchini tanzania amehimiza kutekelezwa haraka mradi huo ili kuwanufaisha wananchi.

Katibu mkuu wa wizara hiyo alhalil mirza amesema masharti ya utekelezaji wa mradi huo yameshakamilika na wanasubiri wataalamu kuanza kazi.

Katika mazungumzo hayo balozi wa india nchini tanzania sandeep arya amesema wataanza kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa mamlaka ya maji zawa na ni mpango wa ushirikiano kati ya nchi hiyo na zanzibar.

chanzo:Zbc.

Comments