
Rais wa Taasisi hiyo Bwana Matthew McLean alitoa kauli hiyo wakati
alipofanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi hukoVuga Mjini Zanzibar.
Mazungumzo hayo pia yalijumuisha Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na
Mazingira Mh. Salama Aboud Talib, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na
Usarifishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum pamoja na watendaji wakuu
wa baadhi ya Taasisi za Serikali.
Bwana Matthew alisema Endsight imekuwa ikitoa ushauri wa Kitaalamu
katika fani ya uhandisi katika kuona kiwango cha miundombinu
kinachowekwa kwenye miradi inayohusika zaidi na masuala ya uhandisi
inatekelezwa katika hadhi na daraja inayotakiwa kitaalamu.
Alisema miundombinu ya bara bara na Mawasiliano , kilimo ikiwemo pia
miradi ya huduma za maji safi na salama inahitaji uangalizi sahihi
katika uanzishwaji wake ili wakati inapoanza kufanya kazi itoe huduma
sahihi iliyokusudiwa kitaalamu.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alisema Mataifa, Taasisi pamoja na Mashirika rafiki yana fursa za
kusaidia au kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika
kuwaletea maendeleo Wananchi wake.
Balozi Seif alimuhakikishia Rais huyo wa Taasisi ya Ushauri ya
Endesight ya Marekani iliyo chini ya Shirika la Changamoto ya Milenia ya
Marekani kwamba Zanzibar iko tayari kushirikiana kwa kina na Taasisi au
Nchi yoyote iliyo tayari kusaidiamipango ya Maendeleo.
Naye Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud
Talib pamoja na watendaji wa Serikali walimueleza Bwana Matthew kwamba
Zanzibar bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na
salama katika baadhi ya maeneo.
Waziri Salama alisema nguvu za washirika wa maendeleo zinahitajika
katika kuunga mkono sekta hiyo licha ya juhudi kubwa inayoendelea
kuchukuliwa na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kuongeza nguvu
kwenye mindombinu ya Sekta ya Maji Nchini.
Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya Endsight iliyo
chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Milenia la Marekani {
MCC } Bwana Matthew yupo Zanzibar kuangalia maeneo ambayo Taasisi yake
inaweza kushirikiana na Zanzibar katika kutoa Ushauri wa Kitaalamu wa
Kiufundi.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Picha: Rais wa Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya
Endsight iliyo chini ya usimamizi wa Shirika la Changamoto ya Milenia
la Marekani { MCC } Bwana Matthew McLean Kulia akizungumza na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Picha: Balozi Seif Ali Iddi Kati kati akiwa katika pamoja na Rais wa
Taasisi ya Ushauri wa masuala ya Uhandisi ya Endsight Bwana Matthew
McLean aliyeko upande wa Kulia yake , Waziri Ardhi Mh. Salama Aboud
Talib Kushoto yake, Naibu Waziri Ujenzi Mh. Mohamed Ahmed Salum wa Pili
kutoka Kushoto pamoja na baadhi ya Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
chanzo:zanzibar24.
Comments