Rais
Magufuli amesema siku hizi siyo vijana peke yao wanao haribu wanafunzi,
na kwamba wapo wazee walioko shapu na hawapitwi kuwapa mimba wanafunzi,
na kuwataka wenye tabia hiyo waache kwa sababu watafungwa kwa miaka 30.
Rais
John Magufuli amesema wanaowapa mimba wanafunzi hawana budi kufungwa
miaka 30 ili kukomesha suala hilo na kuwapa fursa watoto wasome kwani
hao ndiyo viongozi wa kesho.
Rais
amezungumza hayo jana wakati wa uzinduzi wa barabara Kaliua, mjini
Tabora, ambapo aliweka wazi kwamba wanaowapa mimba watoto wa shule siyo
vijana pekee bali wapo wazee nao wameingia kwenye mkumbo huo hali
ambayo inawafanya mabinti washindwe klumaliza elimu ya sekondari.
“Wazee
siku hizi wapo shapu kuliko vijana, wanawapa mimba wanafunzi, muwaache
wasome, ukimpa mimba mwanafunzi unafungwa miaka 30 nguvu zako zikaishie
gerezani,” amesema na kuwataka wanafunzi kusoma ili watimize ndoto zao.
".....Soma kwanza, usipate mimba ukiwa shule, subiri umalize sekondari ndipo upate mimba,” amesema.
Pamoja na hayo Mhe. Magufuli amesema kuwa serikali yake imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa kitanzania elimu.
"Tumeamua
kutoa elimu ndiyo maana tumetenga bilioni 18.777 tunataka watoto wasome
na wasipate mimba, naomba wajiepushe na mimba mpaka watakapotimiza
malengo yao," aliongeza.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments