Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo muhammed ali amesema
adhabu hiyo imetolewa baada ya upande wa mashitaka kuthibitisha kosa
dhidi ya mshitakiwa huyo.
Mshitakiwa huyo mkaazi wa muyuni c mwenye umri wa miaka 70,
ambae ni
mjomba wa mtoto aliyefanyiwa ukatili huo, pia ametakiwa kulipa faini ya
shilingi milioni 20 na akishindwa atumikie tena chuo cha mafunzo miaka
miwili na kufanya muda wa kifungo kuwa miaka saba.
Hakimu huyo amemtaka mshitakiwa kulipa fidia ya shilingi milioni tano kwa mtoto huyo mwenye umri wa miaka kumi na nne.
Awali baada ya mahakama kumtia hatiani mshitakiwa huyo upande wa
mashitaka unaongozwa na mwanasheria kutoka ofisi ya mkurugenzi wa
mashitaka ( dpp) uliiomba mahakama kutoa adhabu kali kutokana na vitendo
hivyo kukithiri katika jamii.
Kwa upande wa wakili wa utetezi wa mshitakiwa huyo shaibu ibrahim
aliiomba mahakama kutoa adhabu kwa mshitakiwa huyo ya kutumikia jamii
kutokana na kuwa na umri mkubwa na hali yake ya kiafya sio nzuri.
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo tarehe 20 mwezi wa 11 mwaka jana
mshitakiwa khalid juma huko mutuni c alimuingilia mtoto wa kike mwenye
umri wa miaka 14, ambapo jumla ya mashahidi 6 waliweza kutoa ushahidi
wao mahakamani hapo..
chanzo:Zbc.
Comments