Mwanamke apokea vitisho kwa kuikojolea bendera ya Marekani.

Emily Lance alipokea vitisho vya mauaji katika mtandao wa kijamii baada ya kuchapisha video ambayo akiikojolea bendera ya Marekani ametoa wito kwa watu kutoilenga familia yake akisema hawaungi mkono tendo lake.

Katika kanda hiyo ya video, Bi Lance anaonekana akisimama juu ya choo ambapo bendera ya Marekani imewekwa na kuikojolea kupitia usaidizi wa chombo ambacho kinawasaidai wanawake kufanya hivyo wakiwa wamesimama.

Chini yake aliandika maneneo ya kuitusi bendera hiyo.
Baadaye aliwataka wanaopinga wazo lake kutowalenga watu wasio na hatia akisema hakuna hata mtu mmoja katika familia yake anayeunga mkono wazo lake.
chanzo:zanzibar24.

Comments