
Kwa mujibu wa Daily Maily, chanzo kimeeleza kuwa mwanamke huyo
anadaiwa alikuwa ndani ya chumba kimoja ghorofani na mume wa mtu. Lakini
mke wa mwanaume huyo alirejea mapema zaidi ya walivyotarajia, hivyo
aliamua kupitia dirishani kuokoa maisha yake.
Katika kipande cha video kilichosambazwa kwenye mitandao, umati
mkubwa wa watu ulikuwa chini ukimtazama, kabla ya baadhi ya wanaume
kuweka ngazi ili kumuokoa mwanamke huyo aliyekuwa ananing’inia akivalia
mavazi mekundu.
Hata hivyo, haikufahamika mara moja kiasi cha maumivu au majeraha
ambayo mwanamke huyo aliyapata kutokana na tukio hilo la hatari.
Video iliyowekwa mtandaoni kuhusu tukio hilo ilikuwa maarufu ndani ya muda mchache ikipata maelefu ya watazamaji.
Hata hivyo, kulikuwa na taarifa nyingine kinzani kuwa huenda mwanamke
huyo alikuwa akisafisha madirisha ya nyumba hiyo, taarifa ambazo
zimechukuliwa kama tetesi.
chanzo: dar24.
Comments