Muumini
wa kanisa Katoliki, Adrian Mpande amepigwa risasi mbili akiwa anasubiri
kuingia kanisani katika Parokia ya Kibangu wilaya Ubungo jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa George Ng’atigwa ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa
Mpande alikuwa akisubiri kuingia kanisani majira ya saa tatu asubuhi
lakini alikuja mtu mmoja aliyekuwa anatembea kwa miguu na kumpiga risasi
ubavuni na mkononi, hali iliyosababisha aanguke na kupoteza fahamu.
Alisema
kuwa mtu huyo alikimbia lakini watu waliokuwa maeneo hayo walifanikiwa
kumkamata baada ya kuishiwa risasi wakati akijaribu kuwatishia.
Aliongeza
kuwa baada ya kumkamata mtu huyo, waliwasiliana na jeshi la polisi
ambalo lilifika na kuondoka naye kwa ajili ya taratibu za kisheria na
kwamba majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada
ya kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati iliyokuwa karibu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Suzan Kaganda
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali
unaonesha kuwa limetokana na ugomvi wa kifamilia.
“Mtuhumiwa
tunaye tunaendelea kumhoji na aliyejeruhiwa yuko hospitali anaendelea
na matibatu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,” Kamanda Kaganda anakaririwa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments