Miundombinu ya barabara yazidi kuimarishwa Zanzibar.

Wizara ya  Miundombinu ,mawasiliano na uchukuzi imeanza ujenzi wa barabara ya kizimbani hadi kiboje  kwa kiwango cha fusi ili kuwaondolea   wananchi usumbufu  unaokwamisha shughuli zao  za maendeleo.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari, Wananchi  pamoja na Viongozi wa Jimbo la miwani  wamesema ujenzi wa barabara utaweza kuleta faraja waliokuwa wanaitafuta kwa muda mrefu kwani tatizo la barabara hiyo  ilipelekea   kusitisha shughuli zao mbalimbali  za kiuchumi  pamoja na kukosekana kwa daladala za abiria.


Kwaupande wake Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Mustafa Jumbe amesema  tayari serikali imeshaanza hatua za  awali za kuitengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha fusi  ili kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi.

Amesema pia kukamilika kwa barabara hiyo kutawawezesha wananchi kusafirisha mazao wanayozalisha kijijini hapo pamoja na kurahisisha huduma nyengine za kijamii ikiwemo upatikanaji huduma za hospital zilizositishwa kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni kwa kiwango cha kifusi  ambayo  inaurefu wa kilomita  7.5 kutoka kizimbani, miwani hadi kiboje.
chanzo: Zanzibar24

Comments