Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo polisi na watendaji wa
mahakama mratibu wa jumuiya kwa watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar
Khamis Abdallah amesema jumuiya hiyo inachukua hatua mbalimbali ili
kuhakikisha wanapata haki zao.
Naibu katibu wa jumuiya hiyo Juma Salum amesema polisi na watendaji
wa mahakama wanapambana na matatizo mengi katika utekelezaji wa kazi zao
katika kuwapatia wanachi haki zao.
Washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa mfumo halisi wa sheria
unavikwazo kwa watu wenye ulemavu kupata haki zao, hivyo wameomba kuwepo
kwa ushirikiano kuanzia kwa wananchi hadi ngazi ya mahakama ili
kuwasaidi kupata haki zao.
chanzo:Zbc.
Comments