MIKAKATI ITAKAYOWAWEZESHA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI KUWEZA KUMILIKI NYUMBA ZITAKAZOJENGWA NA SERIKALI.

Shirika la nyumba zanzibar limeandaa mikakati itakayowawezesha wananchi wenye kipato cha chini kuweza kumiliki nyumba zitakazojengwa na serikali, tofauti na ilivyo sasa.

Akipokea mpango mkakati wa miaka mitano wa shirika hilo mkurugenzi mkuu moh’d hafidh, amesema licha ya kuwepo ujenzi wa makaazi unaoendelea katika eneo huru la vitega uchumi fumba na kwengineko, lakini kwa mwananchi wa kawaida itakuwa vigumu kuweza kumiliki kutokana na ukubwa wa gharama.


Hivyo amesema kupitia mpango huo utawezesha wananchi wa kipato cha chini kuweza kumili na kukodishwa nyumba nyuba hizo kwa kadiri ya uwezo wao.

Katibu mkuu wizara ya ujenzi, mawasiliano na usafirishaji, mustafa aboud jumbe, amelitaka la nyumba kutumia vyema rasilimali zake za majengo kibiashara ili liweze kujiendesha, huku likiangalia zaidi wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu gharama za makaazi.

Mpango huo wa mkakati umewasilishwa na mtaalamu kutoka kampuni ya ict kupitia mradi wa miundombinu.
chanzo:Zbc.

Comments