
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi,dk.Mpola Tamambele amesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha mama mjamzito ,mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma za afya bure .
WAZIRI wa afya, jinsia ,wazee na watoto ,Ummy Mwalimu amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo haraka iwezekanavyo huku uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili ukiendelea.
Aidha kaimu mkurugenzi huyo ametakiwa kuwafuatilia watumishi wa afya waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 katika kituo hicho ili apate huduma .
Waziri wa afya alitoa amri hizo alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi ,kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo ,Hamoud Jumaa .
Waziri Ummy alisema hatokubali kuona baadhi ya watumishi kwenye vituo vya afya ,zahanati na hospitali wanakiuka maagizo ya serikali ingawa hakuwa na mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu hilo.
Amri hiyo ilitolewa kufuatia malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni yakiwemo madawa na vifaaa tiba ,pamba na gloves kwa gharama ya sh .180,000 ili aweze kujifungua.
“Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho ” “Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika .” alisema Ummy .
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi .
Nae mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na malalamiko mengi hususani kwa akinamama na wazee kulipishwa fedha za dawa na vifaa tiba hivyo anamtaka waziri Ummy kuendelea kushirikiana nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi.
chanzo:zanzibar24.
Comments