MASHEHA WAMETAKIWA KUWAFICHUA WATU WANAOTUMIA BANDARI BUBU KWA VITENDO VYA KIHALIFU.

Masheha wa mkoa wa kaskazini unguja wametakiwa kuwafichua watu wanaotumia bandari bubu kwa vitendo vya kihalifu.

Akizungumza na masheha naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa, serikali za mitaa na idara maalum za smz mhe: shamata shaame khamisi amesema bandari bubu nyingi nchini zinatuhumiwa kutumika kwa kusafirishia dawa za kulevya,kusafirisha karafuu kwa njia za magendo.


Amewataka masheha na wananchi kushirikiana katika kuwafichua wahalifu wanao jihusisha na vitendo hivyo ili serikali iwachukulie hatua za kisheria.

Masheha wa mkoa huo wamesema watahakikisha wanatekeleza kwa vitendo maagizo hayo na kuwaomba wananchi kuongeza ushirikiano ili kutokomeza vitendo vya kihalifu nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa tawala za mikoa khalid abdalla omar amewataka masheha hao kusimamia vyema kazi za serikali ili kuimarisha huduma za jamii.
chanzo:Zbc.

Comments