
Mama Advera Kyaruzi ambaye awali alidhulumiwa kiasi cha shilingi
milioni 10 kabla ya kurudishiwa baada ya Rais Dkt. John Magufuli
kuingilia kati.
Akizungumza na TBC Jijini Arusha, Advera Kyaruzi amesema alifikia
uamuzi wa kwenda Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi Siku ya Mei
Mosi kumuona Rais Magufuli baada ya kukosa msaada katika ngazi
mbalimbali na Rais kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA kushughulikia suala
hilo.
Kyaruzi amesema aliamua kutafuta haki yake kwa kumuona Rais John
Magufuli kutokana na nyumba yake kutishiwa kuuzwa pamoja na kufunguliwa
kesi ya kudaiwa fedha ambazo alikopa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema
viongozi, wapo kwa ajili ya kuhudumia wananchi wanyonge wamekuwa
wakidhulumiwa mali zao.
chanzo: zanzibar24.
Comments