Mafunzo na utafiti wa maradhi ya minyoo.

Mafunzo na utafiti wa maradhi yasiyopewa kipaombele kwa wataalamu mbalimbali wa afya yamesaidia kupungua maradhi hayo zanzibar.

Akizungumza na zbc kwenye mafunzo ya kumi ya kimataifa ya maradhi yasiyopewa kipaombele, afisa mtendaji mkuu wa maabara ya afya ya jamii chake chake dk. Said mohamed ali amesema tokea kunzishwa kwa mradi huo maradhi ya minyoo yalikuwa ni asilimia 85 na kichocho kilikuwa kati ya asilimia 8 mpaka 30 ambayo zaidi yakiwasumbua watoto wa skuli.


Mshiriki wa mafunzo hayo veronika kabona kutoka wizara ya afya tanzania bara amesema kupitia mafunzo hayo watajifunza njia mpya za kupambana na maradhi hayo ambayo ni tatizo kubwa ndani ya jamii.

Mafunzo hayo ya wiki tatu yaliyofunguliwa na katibu mkuu wizara ya afya asha ali abdalla ambayo yanasaidia kubadilishana uzowefu katika taaluma ya afya ikiwemo utafitu yanashirikisha nchi kumi zikiwepo za europia na afrika yanalengo la kuondosha kabisa tatizo hilo katika jamii.

chanzo:Zbc.

Comments