Upungufu wa vifaa tiba na dawa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Rukwa, umetajwa kukwamisha jitihada za madaktari bingwa kutoa tiba kwa wagonjwa wanaohitaji huduma yao.
Hali hiyo inatajwa kuwa ndicho chanzo cha wagonjwa wengi kupewa rufaa.
Uhaba wa vifaa tiba umesababisha madaktari hao kushindwa kufanya kazi licha ya mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kuwapeleka mkoani Rukwa kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu kama vile moyo, madaktari bingwa wa watoto, mfumo wa mkojo, pua, koo, na masikio sambamba na madaktari bingwa wa afya ya uzazi na akina mama.
Akizungumza leo , Ijumaa, Julai 7, daktari bingwa wa moyo, Issakwisa Mwakyula, amesema kwamba kati ya wagonjwa wapatao 200 ambao amewatibu maradhi hayo, asilimia tano wamepewa rufaa ya kwenda hospitali za rufaa, Mbeya na Muhimbili, Dar es salaam kwa ajili ya vipimo na kupata huduma ya dawa kwa kuwa dawa hazipo katika hospitali hizo.
"Sisi tulikuja na vipimo vyetu lakini kuna vipimo vingine havipo hapa hospitalini, pia dawa hazipatikani kiasi kwamba tunawaeleza wagonjwa waende kununua nje ya hospitali," amesema.
Kwa upande wake, Dk. Benedick Ngalyale ambaye ni bingwa wa magonjwa ya koo, pua, na masikio, amesema kutokana hospitali hiyo kukosa vifaa tiba wagonjwa wengine wameandikiwa rufaa ya kutoka nje ya mkoa huo kwa ajili ya tiba zaidi.
Amesema kati ya wagonjwa 220, wagonjwa 10 walifanyiwa upasuaji mkubwa na 20 walifanyiwa upasuaji mdogo lakini amebaini tatizo la magonjwa hayo ni kubwa kwa wakazi wa mkoa huo.
Hivyo, kutokana na upungufu huo, bado baadhi ya wagonjwa watalazimika kutembea umbali mrefu ili kupata matibabu hali ambayo inakwenda kinyume na dhamira ya NHIF ya kutaka wapate tiba pasipo kutembea umbali mrefu.
Kwa mujibu wa Mlezi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa, Zebrina Malamsha, wagonjwa 850 wanaosumbuliwa na maradhi sugu mkoani Rukwa wamenufaika na mpango huo wa kufikiwa na madaktari bingwa na kupata tiba ya maradhi hayo.

chanzo:Mwananchi.
Comments