
Wakizungumzia operesheni hiyo wafanyakazi wa mabasi na mawakala
wamekuwa na maoni tofauti wakati wengine wakidai kutopatiwa muda wa
kutosha kufanya marekebisho wengine wameunga mkono zoezi hlo huku
abiria wakieleza walivyoathirika.
Katika ukaguzi huo maafisa wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama
barabarani wamegundua makosa mengi yakiwemo kukosa mikanda ya abiria
uchakavu wa maumbo ya magari na kati ya zaidi ya mabasi hamsini
yaliyokaguliwa madereva watano wenye makosa sugu wamefikishwa
mahakamani.
chanzo: zanzibar24.
Comments