
Kwa mujibu wa utafiti huo mabaki ya mtu huyo ni ameishi katika karne ya 16 na inawezekana kuwa ni wageni kutoka nchini Ureno.
Mkuu wa Divisheni na Mambo ya Kale, Abdalla Khamis Ali alisema hayo
alipokuwa akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake Forodhani, akielezea
utafiti huo unaoendelea katika eneo hilo.
Alisema mabaki ya mwili wa binaadamu huyo yalikutwa pembezoni mwa
ukuta wa kanisa na imethibitika kuwa alikuwa ni muumini wa dini ya
kikiristo.
Alisema suala la imani yake limebainika kufuatia kukutwa akiwa na
msalaba, huku pia mwili wake ukiwa umezikwa miguu kuelekea mashariki na
kichwa kuelekea magharibi.
Mkuu huyo alifahamisha kuwa mwili huo unakisiwa kuwa ni wa mtu
mwanamke, lakini utafiti zaidi utafanyika ili kuuweza kuufanyia
uchunguzi mwili huo.
Aidha alifahamisha kuwa ndani ya mabaki hayo wamebaini nembo ya kopa,
hivyo kutokana na sababu tatu hizo ndizo zilizowafanya kubaini kuwa
maiti hiyo ilikuwa ya kikristo.
“Maiti hii inawezekana ikawa ya mwanzo ya wareno iliyozikwa zaidi ya
miaka 500 iliyopita katika eneo hilo, lakini pia inawezekana ikawa mtu
huyo alikuwa kiongozi katika kanisa hilo,”alisema.
Alisema mbali ya kukuta mabaki ya mwili huo pia wamekuta mabaki ya
vyombo vya kigae ambavyo vinasadikiwa kutoka nchi za nje vilivyokuwa
vikitumiwa na watu waliokuwa wakiishi kipindi cha karne ya 11,12 au 13.
Hata hivyo alifahamisha kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kutumia vitu
vya kisasa walifanikiwa pia kugundua vitu vingine kadhaa vilivyokuwepo
ndani ya Ngomekongwe ikiwemo kuta za majengo mbalimbali yaliyojengwa na
Wareno ikiwemo kanisa na nyumba nyengine ambazo walikuwa wakizitumia kwa
shughuli zao mbalimbali.
chanzo: zanzibar24.
Comments