
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho Vuga
Mjini Zanzanzibar ,Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF Maalim Seif
Sharif Hamadi amesema kwa mujibu wa sheria na katiba ya Chama hicho
wabunge ni lazima watambulike na baraza hilo ndipo kutangwazwa na tume
ya Uchaguzi.
Maalim Seif amesema Baraza hilo litaendelea kuwatambua wanachama hao
kutokana na kuwa ni wanachama halali wanaotambulika kisheria, licha ya
kuwa tume ya Uchaguzi imesha tangaza majina mapya yatayoweza kujaza
nafasi zilizoachwa wazi na wanachama waliofukuzwa.
Amesema mbali na wabunge hao baraza hilo pia litaendelea kuwatambuwa
madiwani wa Viti maaalum akiwemo Mh. Leila Hussein Madibi anaetokea
Ubongo na Elisabeth Mangwanja anaetokea Temeke licha ya kuwekewa
vikwazo vya kutotambuliwa na uongozi wa Prof. Ibrahim Lipumba ambao ni
feki na hautambuliki kisheria.
Aidha Baraza hilo limesema litaendelea kuwaunga mkono wananchama hao
katika kutafuta haki yao ya msingi kwa hatua ya kupeleka malalamiko yao
mahakamani ili waweze kuwatumikia wananchi katika keleta maendeo ya nchi
na Chama hicho.
Maalimu Seif ametowa wito kwa Jumuiya za kimataifa kuiwekea vikwazo
vya kiuchumi Tanzania pamoja na kuitenga kisiasa na kidiplomasia hadi
watawala watakapo heshimu haki za binaadamu na utawala wa sheria.
Hata hivyo amewatowa wasi wasi wanachama wa CUF kuendelea kukiunga
mokono chama hivyo ili kiweze kuwaletea maendeleo katika nchi.
chanzo:Zanzibar24.
Comments